Kwa mujibu wa habari hizo, hatua hiyo imekuja kufuatia Kamati teule ya Bunge iliyoundwa kuchunguza sakata hilo kutoa majibu yaliyowahusisha vigogo hao, hali iliyomfanya Waziri Mkuu mpya, Mizengo Pinda kuahidi bungeni kushughulikia mapendekezo ya kamati hiyo."Kinachofanyika sasa na mamlaka husika ni kuchunguza kwa kina kila
anayetajwa kuhusika na suala la Richmond, anamiliki mali zipi,ziko wapi na kiasi gani cha fedha alizonazo katika benki zipi nchini, na hata nje ya nchi.
“Hii ni katika kubaini ukweli wa ufisadi unaodaiwa kuwepo,” kilisema chanzo hicho na kisisitiza kuwa kazi hiyo tayari imeshaanza.
Hata hivyo, habari zinasema kuwa hiyo ni kazi ngumu, hasa ikitiliwa maanani kuwa baadhi ya watuhumiwa wa sakata la Richmond ni wafanyabiashara ambao wana fedha nyingi ambazo haitakuwa rahisi kujua kama zilitokana na ufisadi au la!Lowassa, Karamagi na Dk. Msabaha wanatajwa katika sakata la zabuni ya umeme wa dharura wa Kampuni ya Richmond na kuzua mjadala mkubwa uliosababisha kuundwa kwa tume ya uchunguzi iliyokuwa chini ya Mbunge wa Kyela, Dk. Harrison Mwakyembe.
Kamati ya Dk. Mwakyembe iliwahusisha kwa namna moja au nyingine vigogo hao, hatua iliyowafanya kujiuzulu, akiwemo aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa jambo lililosababisha baraza zima la mawaziri kuvunjwa na Rais Jakaya Kikwete.
Akiahirisha bunge wiki iliyopita, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda alisema atashughulikia suala la kashfa ya Richmond na akaahidi kuunda tume maalumu ya kufuatilia sakata hilo.
Alisema wajumbe wa tume hiyo watatoka Ikulu, ofisi yake (Waziri Mkuu), Menejimenti ya Utumishi, TAMISEMI, Tume ya Mipango na Bodi ya Mahesabu mbapo kila ofisi itatoa ofisa mmoja.
Aliwaahidi wabunge kuwa baadhi ya mapendekezo ya kamati ya Mwakyembe watayatolea maelezo utekelezaji wake katika mkutano wa 11 wa bunge utakaofanyika Aprili mwaka huu. Waziri Mkuu Pinda alianza kazi rasmi juzi
(Jumatatu). courtesy of Global Publishers

Subscribe to:
Posts (Atom)